VIDEO: Polisi wasema Mo Dewji alitupwa viwanja vya Gymkhana

What you need to know:

Dakika chache baada ya mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’  kupatikana, Jeshi la Polisi Tanzania limesema watekaji walimtupa katika viwanja vya Gymkhana katikati ya Jiji la Dar es Salaam


Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji 'Mo Dewji' alitupwa kwenye Viwanja vya Gymkhana katikati ya jijini la Dar es Salaam.

Akizungumza leo Jumamosi Oktoba 20, 2018 Mambosasa amesema polisi walipata taarifa leo saa nane usiku kuwa mfanyabiashara huyo amepatikana na watekaji walimchukua kwenye gari waliyotumia kumteka na kumtupa katika viwanja hivyo.

“Polisi tulipata taarifa kwamba amepatikana, watekaji walimchukua kwenye gari ile ile waliyotumia kumteka na kwenda kumtupa katika viwanja hivyo,” amesema Mambosasa.

“Tangu alivyotekwa pale hoteli ya Collesium (alfajiri ya Oktoba 11, 2018) gari ya watekaji iliondoka kasi na baada ya dakika  15 Dewji alijikuta amewekwa kwenye chumba akiwa amefunikwa  ili asiwatambue watekaji.”

Amebainisha kuwa mfanyabiashara huyo amewaeleza kuwa watu waliomteka walikuwa wakizungumza moja ya lugha za Afrika Kusini.

“Baada ya kumhoji ameeleza kuwa alitambua lugha walizokuwa wakizungumza kwamba ni kama za Afrika Kusini. Mashaka yetu kuwa waliofanya tukio hili sio Watanzania yamethibitishwa na Dewji mwenyewe,” amesisitiza.

 

VIDEO: Familia ya 'Mo Dewji': Tunamshukuru Rais Magufuli