Umasikini wa wafugaji ni kuthamini idadi ya mifugo kuliko fedha, mali

What you need to know:


Umasikini wa wafugaji ni kuthamini idadi ya mifugo kuliko fedha, mali

Inashangaza kuona kuwa Tanzania ni nchi ya tatu barani Afrika kwa wingi wa mifugo ya asili lakini wafugaji wengi wanaishi maisha duni. Serikali imeshindwa pia kupata kikamilifu matunda ya kuwepo kwa raslimali hii.
Kwa mujibu wa ripoti ya ufugaji ya Wiara yaMifugo ya mwaka 2013,  zaidi ya kaya 2.3 milioni zilikuwa zinategemea ufugaji kama chanzo kikuu cha kipato.
Pamoja na ukweli huo, ripoti hiyo inahitimisha kwa kueleza kwamba mchango wa mifugo ni mdogo sana katika kubadili maisha ya wafugaji na kuchangia ipasavyo katika pato la taifa.
Kulingana na takwimu hizo, ng’ombe wanaongoza kwa wingi wakifuatiwa na mbuzi, kondoo na nguruwe.
Ripoti hiyo inasema idadi ya ng’ombe 22.8 milioni, mbuzi 15.5 milioni, kondoo 6.9 milioni na nguruwe 2.1 milioni.
Pamoja na uwepo wa mifugo hiyo bado haujakidhi mahitaji ya soko la nyama wala maziwa. Katika kipindi cha utafiti ni lita 48,079 pekee ndizo zilikamuliwa kwa siku na tani 81,311 za nyama kwa mwaka zinazotokana na uchinjaji ng’ombe 4,929 mbuzi na kondoo 639  na nguruwe 1,839.
Wakati mifugo hiyo ikitegemewa na nchi nyingine, kuwa chachu ya kuinua uchumi wa wafugaji na na taifa kwa ujumla, kwa Tanzania ni balaa linaloleta maafa kila uchao.
1.    Nini kifanyike ili mifugo iweze kuleta tija kwa wananach na hasa wafugaji amabao hutegemea mifugo kama njia kuu ya kipato
2.    Tatizo la migogoro tunaweza kulihihushisha moja kwa moja na wafugaji wengi kuhama kutoka eneo moja hadi lingine kutafta malisho..? nini suluhisho la kudumu katika kupunguza kuhama kwa wafugaji..?